AAR Insurance (Tanzania) Limited ni sehemu ya Kampuni ya AAR Holdings, ambayo ndio Kampuni kubwa na yenye mafanikio makubwa zaidi kwa Kampuni Binafsi za Bima ndani ya Afrika Mashariki. Nchini Tanzania, Makao Makuu yake yapo Dar es Salaam, pia in ofisi za mauzo Arusha, Mwanza, Dodoma na Zanzibar.
AAR Insurance Tanzania Limited inatoa nafasi sawa za ajira kwa wanaume na wanawake wenye sifa.
Kwa Kuzingatia Malengo ya kuwa na uangalizi mzuri na wa mara kwa mara katika maeneo makuu ya utendaji kazi, tunatarajia kuajiri nafasi ifuatayo:
Afisa Mauzo
Kufanya uchunguzi, kutafiti na kutafuta maeneo mapya ya kibiashara ili kuiwezesha kampuni kutimiza malengo yaliyowekwa ya ukusanyaji mapato.
Afisa Mauzo atakeajiriwa atafanya kazi zake Dodoma na ataripoti kwa Meneja Uendelezaji Biashara ambaye anasimamia office za mawakala
Muombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo
a) Kiwango cha Elimu
Shahada ya kwanza au Stashahada (degree and /or Diploma) katika fani yoyote ile.
b) Taaluma
Mwenye cheti cha COP atapewa nafasi zaidi
c) Ujuzi/uwezo Binafsi
Waombaji wanatakiwa kuambatanisha maombi yao na maelezo binafsi (CV) pamoja na vivuli vya vyeti vyao na watume moja kwa moja ofisini:
Watume Kwa:
Meneja Mauzo
AAR Insurance (Tanzania) Ltd
Kazimoto Shoppers Plaza Ground Floor, Mkabala na TRA
Dodoma
Au watume kwa njia ya email kwa: dodoma@aar.co.tz
Tarehe ya mwisho ye kupokea maombi ni siku ya ijumaa tarehe 03 Mei, 2019