Bodi ya chama cha ushirika wa akiba na mikopo Lulu(Lulu Saccos Ltd) MBR.737 kilichopo Jiji la Mbeaya maeneo ya Soweto kata ya Ruanda kinatoa tangazo la kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Afisa Mikopo(Nafasi 1)
Sifa
- Awe na umri kuanzia miaka 25 hadi 50
- Awe na elimu ya sekondari
- Awe na shahada ya uhasibu, ushirika, na masoko, na usimamizi wa fedha kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali
- Awe hajawahi kufukuzwa kazi mahala popote
- Awe mtu wa kujituma
- Awe mtu anayejisimamia mwenyewe
- Awe anajua kutumia kompyuta
- Awe mtanzania anayeishi katika jiji la Mbeya
- Awe mzaliwa/mwenyeji wa mkoa wa Mbeya
Kazi
- Kutunza na kutoa fomu za maombi ya mikopo
- Kupitia fomu za maombi ya mikopo
- Kutembelea maeneo ambako waombaji mikipo wanapofanyia biashara zao
- Kuandaa vikao vya kamati ya mikopo
- Kuhakikisha mikopo iliyoidhinishwa inatolewa kwa wakati
- Kufuatilia marejesho ya mikopo
- Kutoa elimu ya biashara kwa waombaji mikopo
- Kufanya kazi zingine atazopangiwa na mwajiri wake
KAZI HII NI YA KUJITOLEA KWA MUDA WA MIEZI MITANO(5) BAADA YA HAPO ATAAJIRIWA KAMA ATAKUWA AMEKIDHI VIGEZO
Utaratibu wa kuomba
- Mwombaji anatakiwa kuambatanisha picha mbili passport size
- Mwombaji atatakiwa kuambatanisha vivuli vya vyeti vya kuzaliwa na vya masomo
- Mwombaji aambatanishe CV yake wakati wa kuomba kazi
- Mwombaji aonyeshe mawasiliano yake bayana
- Mwombaji atakayefaulu kwa awamu ya kwanza ataitwa kwenye usaili
- Mwombaji atakeyeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili
- Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usaili
- Maombi yatumwe kwa:-
MWENYEKITI WA BODI
CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO LULU
S.L.P 3467
MBEYA