Dereva II Tea Board of Tanzania (TBT) Tanzania
Job Type: Full-Time
Closing Date: 30th October 2023
Location: Dar es Salaam, Tanzania

DUTIES AND RESPONSIBILITIES

i.Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;

ii.Kuwapeleka watumishi kwenye maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi;  

iii.Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;

iv.Kutunza na kuandika safari zote katika daftari la safari “Log-book”; 

v.Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali;

vi.Kutoa ushauri wa kiufundi  kuhusu usalama na uendeshaji wa gari; 

vii.Kufanya usafi wa gari; na

viii.Kufanya kazi nyingine kama atakavyopangiwa na kiongozi wake zinazohusiana na elimu na ujuzi wake wa kazi. 

QUALIFICATION AND EXPERIENCE

Cheti cha Kidato cha Nne (Form IV) na Leseni ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria Mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wenye Cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.

REMUNERATION: TGS B