Bodi ya chama cha ushirika wa akiba na mikopo Lulu(Lulu Saccos Ltd) MBR.737 kilichopo Jiji la Mbeya maeneo ya Soweto kata ya Ruanda kinatoa tangazo la kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Meneja (Nafasi 1)
Sifa
- Awe na umri wa miaka kuanzia 30 hadi 50
- Awe na elimu ya sekondari
- Awe na shahada ya uongozi, uhasibu na fedha, biashara na masoko
- Awe ni mtanzania anayeishi katika jiji la Mbeya
- Awe anajua kutumia kompyuta
- Muombaji atakaye kuwa na shahada ya pili itamwongezea sifa
- Awe na uwezo wa kusimamia watendaji walioko chini yake
- Awe mbunifu wa mambo mapya
- Awe anajituma kufanya kazi
- Awe mtu anayejisimamia mwenyewe
- Atawajibika kwa bodi ya chama
- Awe ni mzaliwa/mwenyeji wa mkoa wa Mbeya
- Kazi hii ni ya mkataba wa miaka miwili
Kazi
- Kufanya mawasiliano yote kwa niaba ya chama
- Kuishauri bodi katika shughuli za ujasiliamali
- Kuweka saini kumbukumbu zote kwa niaba ya chama
- Kuishauri bodi kuhusu uajiri na kuendeleza watumishi
- Kusimamia na kuratibu mipango yote ya uchumi ya chama
- Kutayarisha taarifa za mwezi, robo, nusu na mwaka
- Kuwa mratibu wa vikao vya bodi
- Kuhifadhi nakala ya masharti ya chama
- Kuandaa hesabu za mwaka
- Kutoa taarifa kwa bodi
- Kuwa msimamizi mkuu wa watumishi wa chama
- Kusimamia uendeshaji wa shuuli za chama za kila siku
- Kuhakikisha kuwa chama kinakuwa na fedha za kutosha kwa ajili ya mikopo
Utaratibu wa kuomba
- Mwombaji anatakiwa kuambatanisha picha mbili passport size
- Mwombaji atatakiwa kuambatanisha vivuli vya vyeti vya kuzaliwa na vya masomo
- Mwombaji aambatanishe CV yake wakati wa kuomba kazi
- Mwombaji aonyeshe mawasiliano yake bayana
- Mwombaji atakayefaulu kwa awamu ya kwanza ataitwa kwenye usaili
- Mwombaji atakeyeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili
- Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usaili
- Mwisho wa Kupokea maombi ni tarehe 18/07/2018
- Maombi yatumwe kwa:-
MWENYEKITI WA BODI
CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO LULU
S.L.P 3467
MBEYA