Sanlam Life Insurance (T) Ltd, kampuni inayoongoza nchini Tanzania katika uto aji wa huduma za bima za maisha (Life Insurance) inatangaza nafasi (70) za kazi za Afisa Mauzo (Financial Advisors) katika kitengo cha mauzo kwenye ofisi zake za: Mwanza, Arusha, Mbeya, Zanzibar na Dar-es-Salaam. Wakazi wa mikoa husika na wale kutoka nje ya mikoa hiyo wanaopenda kufanya kazi kwenye kanda ambazo tuna matawi yetu wanakaribishwa kutuma maombi yao.
Sifa za mwombaji:
- Cheti cha kidato cha nne au cha sita
- Cheti au stashahada au shadada ya bima,utawala wa biashara, masoko, mauzo au mafunzo mbadala. . Cheti cha bima (COP) kinapendelewa
- Awe na ari ya kupata kipato kikubwa kwa kufanya mauzo mengi.
- Uzoefu wa kuuza huduma za bima au huduma za kifedha nyinginezo unahitajika.
- Utayari wa kutoa huduma kwa wateja popote pale walipo utazingatiwa.
- Awe na uwezo wa kuzungumza na kuandika Kiswahili na Kiingeza fasaha.
- Awe na uwezo kufanya hesabu za kujumlisha kwa usahihi
- Awe na uwezo wa kushawishi na kujenga mahusiano
- Awe tayari kufanya kazi kwenye tawi lililopo mbali na makazi yake ikibidi.
Kama una sifa hizo hapo juu tuma maombi yako wanayotaja tawi mojawapo kati ya yaliyotajwa hapo juu ambalo unapenda kufanya au lete kwa mkono kwa:
Mkuu wa Utumishi na Utawala,
Sanlam Life Insurance (T) Ltd, P.o box 22229 Mtaa wa Ohio, Jengo la Amani Place Ghorofa ya 9, Dar-es-Salaam.
Baruapepe: recruitment@sanlamlifeinsurance.co.tz
Maombi yatufikie kabla ya tarehe: 26/11/2021
ISHI KWA KUJIAMINI!