Afisa Mikopo Lulu Saccos Ltd Mbeya
Full-Time
18th July 2018
2844

Bodi ya chama cha ushirika wa akiba na mikopo Lulu(Lulu Saccos Ltd) MBR.737 kilichopo Jiji la Mbeaya maeneo ya Soweto kata ya Ruanda kinatoa tangazo la kazi kwa nafasi zifuatazo:-

Afisa Mikopo(Nafasi 1)

Sifa

  • Awe na umri kuanzia miaka 25 hadi 50
  • Awe na elimu ya sekondari
  • Awe na shahada ya uhasibu, ushirika, na masoko, na usimamizi wa fedha kutoka vyuo vinavyotambuliwa na serikali
  • Awe hajawahi kufukuzwa kazi mahala popote
  • Awe mtu wa kujituma
  • Awe mtu anayejisimamia mwenyewe
  • Awe anajua kutumia kompyuta
  • Awe mtanzania anayeishi katika jiji la Mbeya
  • Awe mzaliwa/mwenyeji wa mkoa wa Mbeya

Kazi

  • Kutunza na kutoa fomu za maombi ya mikopo
  • Kupitia fomu za maombi ya mikopo
  • Kutembelea maeneo ambako waombaji mikipo wanapofanyia biashara zao
  • Kuandaa vikao vya kamati ya mikopo
  • Kuhakikisha mikopo iliyoidhinishwa inatolewa kwa wakati
  • Kufuatilia marejesho ya mikopo
  • Kutoa elimu ya biashara kwa waombaji mikopo
  • Kufanya kazi zingine atazopangiwa na mwajiri wake

KAZI HII NI YA KUJITOLEA KWA MUDA WA MIEZI MITANO(5) BAADA YA HAPO ATAAJIRIWA KAMA ATAKUWA AMEKIDHI VIGEZO

Utaratibu wa kuomba

  1. Mwombaji anatakiwa kuambatanisha picha mbili passport size
  2. Mwombaji atatakiwa kuambatanisha vivuli vya vyeti vya kuzaliwa na vya masomo
  3. Mwombaji aambatanishe CV yake wakati wa kuomba kazi
  4. Mwombaji aonyeshe mawasiliano yake bayana
  5. Mwombaji atakayefaulu kwa awamu ya kwanza ataitwa kwenye usaili
  6. Mwombaji atakeyeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili
  7. Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usaili
  8. Maombi yatumwe kwa:-

MWENYEKITI WA BODI

CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO LULU

S.L.P 3467

MBEYA

Application

Sorry, this job no longer accepts new applications.