Dereva The School of St Judes Moshono, Arusha, Tanzania
Full-Time
28th April 2025

Tangazo la Kazi: Nafasi za Udereva (1) 

  

Kuhusu Shule

Shule ya St Jude ni shule inayotoa elimu ya hisani ndani ya Tanzania. St Jude’s inafadhiliwa na wafuasi wa ukarimu kutoka kote ulimwenguni ambao hufanya dhamira yetu ya kuwapa wanafunzi wa Kitanzania mahiri na wanaotoka kwenye mazingira ya kimaskini elimu bure na yenye ubora. 

 

Shule ya St.Jude inayofuraha kutangaza nafasi Moja (1) ya kazi ya Udereva kwa watanzania wenye sifa stahiki. 

 

Kazi na Majukumu  

  • Kuendesha magari ya shule kwa uangalifu na umakini 
  • Kuwa makini na kukagua  mara kwa mara gari ulilokabidihiwa kuhakikisha lipo salama kabla ya na wakati wa kuliendesha 
  • Kutunza taarifa za gari/vipuri/mafuta na mabadiliko yoyote ikiwemo kujaza “log book” kwa usahihi na kwa kila tukio na safari za gari 
  • Kuripoti kwa wakati muda wa gari kukarabatiwa na/au kwenda “service” 
  • Kufuata taratibu sheria kanuni na miongozo ya usalama barabarani 
  • Kutoa ushirikiano kwa mamlaka ya shule na taasisi husika pale linapotokea tatizo kwa gari la shule unaloendesha 
  • Kufuata mipangilio na ratiba za magari na maelekezo ya Dereva Mkuu kuhusu Route za magari 
  • Kushiriki sikukuu na shughuli za kijamii za The School of St. Jude mara zipangwapo 
  • Kutoa taarifa ya maandishi ikiwa gari unaloendesha litapata hitilafu au ajali itakayozuia safari iliyopangwa au ruti kuendelea. 

 

Sifa za Mwombaji 

  • Awe Mtanzania mwenye umri usiopungua miaka 35. 
  • Ajue kusoma na kuandika vizuri kwa Kiswahili. Kuzungumza, kuandika na/au kusoma kiingereza itaboresha ombi. 
  • Awe na leseni hai ya udereva ya daraja “C-plain” 
  •  Cheti cha Udereva kutoka kwenye chuo kinachotambulika 
  • Awe na uzoefu wa angalau miaka miwili (2) kuendesha mabasi   ya shule.  

 

Vigezo na Masharti 

Mwombaji anatakiwa kutimiza masharti yafuatayo kikamilifu 

  • Barua ya maombi iambatanishwe na; 
  • Wasifu binafsi (CV)  
  • Barua ya uhakiki wa leseni kutoka polisi. 
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa 
  • Barua ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtaa anapoishi 
  • Kuambatanisha cheti/nyaraka za kughushi itapelekea kuchukuliwa hatua za kisheria 
  • Maombi yawasilishwe katika Shule ya St. Jude Kampasi ya Moshono kabla au jumatatu, tarehe 28 Aprili 2025. Maombi yatakayowasilishwa baada ya tarehe na muda uliopangwa hayatafanyiwa kazi.  

 

TUTAWASILIANA NA WALE TU WATAKAOKIDHI VIGEZO NA SIFA KWA AJILI YA MAJARIBIO NA MAHOJIANO! 

 

 

ANGALIZO: 

TAFADHALI KUWA MAKINI NA MATENDO YA UDANGANYIFU KATIKA MATANGAZO YA KAZI NA MCHAKATO WA AJIRA. SHULE YA ST JUDE HAIOMBI MALIPO KATIKA HATUA YOYOTE YA MCHAKATO WA KUAJIRI. MAOMBI YOYOTE YA MALIPO YAKATALIWE NA KURIPOTIWA KWA MAMLAKA YA UTEKELEZAJI WA SHERIA ZA MITAA KWA HATUA STAHIKI. 

Application
Login to Quickly Apply