Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam anawatangazia wananchi wote wenye sifa za kuajiriwa kuleta maombi yao ya kazi kwa nafasi zifuatazo:
DEREVA II (DRIVER II)- NAFASI (01) - NGAZI YA MSHAHARA TGS B:
SIFA ZA MWOMBAJI:
(a) Kuajiriwa mwenye Cheti cha kidato cha nne (Form IV) na leseni ya Daraja la E au C1 ya uendeshaji magari ambayo amefanyia kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali. Waombaji wenye cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.
MAJUKUMU YA KAZI:
(i) Kuendesha magari ya abiria na malori,
(ii) Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari
(iii) Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari za kikazi
(iv) Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari
(v) kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali
(vi) kujaza na kutunza tarifa za safari zote katika daftari la safari
(vii) Kufanya usafi wa gari; na
(viii) Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake
MASHARTI YA JUMLA:
(i) Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania wenye umri wa kuanzia miaka 18 usiozidi miaka 45.
(ii) Waombaji wote waambatishe nakala ya Vyeti vya Taaluma, Vyeti vya Kidato cha Nne na Sita, Cheti cha kuzaliwa, picha mbili (2) passport size ya hivi karibuni iandikwe majina ya mwombaji kwa nyuma.
(iii) Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono na mwombaji mwenyewe zikiambatishwa na maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) na namba za simu za kuaminika.
(iv) Testimonials na Provisional Results", Statement of Results, hati matokeo za kidato cha nne (Form IV or VI results slips HAVITAKUBALIWA,
(v) Waombaji waliosoma Nje ya Nchi wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (NECTA)
(vi) Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza. (vii) Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
(viii) Tangazo hili pia linapatikana kwenye Tovuti ya Jiji www.dcc.go.tz
(ix) Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10 Desemba, 2018.
(x) Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika Ofisi za Jiji HAURUHUSIWI,
MAOMBI YOTE YATUMWE KWA NJIA YA POSTA.
MAOMBI YATUMWE KWA:
Mkurugenzi wa Jiji,
Halmashauri ya Jiji.
"Ukumbi wa Jiji"
S.L.P. 9084,
1 Barabara ya Morogoro,
11882 DAR ES SALAAM
5.0 Waombaji waliokidhi sifa wataarifiwa tarehe ya kufanya usaili kwa njia ya maandishi kupitia magazeti yaliyotumika kutangaza nafasi hizi pamoja na simu za mikononi au Tovuti: www.dcc.go.tz
Sipora J.Liana
MKURUGENZI WA JIJI,
HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM