Madereva Simba Logisitics Limited Tanzania
Full-Time
28th May 2020

Kampuni ya usafirishaji ya Simba Logisitics Limited inawatangazia nafasi za kazi kwa madereva wa Malori.

NAFASI: 75

Sifa za Mwombaji

  1. Awe amehitimu na kutunikiwa cheti halali cha kidato cha nne au cha sita. (Mwenye vigezo Zaidi atapewa kipaumbele)
  2. Leseni halali ya Daraja E ambayo haijaisha muda wake.
  3. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na chou cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au chou Kingine kinachotambuliwa na Serikali
  4. Awe amehudhuria mafunzo ya uendeshaji malori ya mizigo (HDV/HGB Professional Driving) Kutoka chou cha NIT
  5. Waombaji wenye cheti cha majaribio ya ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza
  6. Awe na uzoefu wa kuendesha malori ya aina zote (Pulling, semi trella, intersemi, interlink nk)
  7. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani nan amba za simu za kuaminika Pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  8. Awe na hati halali ya kitabu ya kusafiria (Passport mpya ya Kielektroniki)
  9. Cheti cha kutokua na makosa yoyote ya jinai toka polisi (Police Clearance Certificate)
  10. Kadi ya chanjo ya joma (Vaccination Card)
  11. Awe nan amba ya simu yenye mawasiliano ya whatsapp muda wote na yenye uwezo wa kupiga picha nzuri
  12. Waombaji wote wawe ni raia wa Tanzania na wenye umri kati ya miaka 30-45
  13. Aambatanishe cheti cha utumishi kutoka kwa mwajiri wa mwisho

Jinsi ya kutuma

  1. Tuma Barua ya maombi yalioandikwa kwa mkono na iambatanishwe na picha ya mwombaji
  2. Maombi yaambatane na barua ya utambulisho wa serikali za mtaa
  3. Barua ya maombi iambatane nan akala ya vyeti vya taaluma na viambata tajwa hapo juu
  4. Nakala ya cheti cha kuzaliwa au kitambulisho cha uraia
  5. Maombi yote yawasilishwe kwa PDF kupitia Email julia@simba-logistics.com nakala kwa Michael@simba-logistics.com au yaletwe kwa mkono katika Ofisi zetu zilizopo Tabata Matumbi, Plot 1000, Nelson Mandela Road, Dar es Salaam.
  6. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
  7. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28 Mwezi Mei 2020 saa 10 jioni.

 

Kwa maelezo Zaidi wasiliana na amba: 0714-592743

Application

Sorry, this job no longer accepts new applications.