MADEREVA WA MAGARI MAKUBWA (NAFASI 80)
GALCO Limited ni kampuni inayouhusika na usafirishaji wa mizigo tofauti ndani nan je ya nchi.
GALCO Limited inahitaji madereva wenye WELEDI, USOEFU NA UADILIFU wa hali ya juu usiotiliwa shaka na mtu au taasisi yoyote ndani na nje ya nchi.
Waombaji wa nafasi hizi wanatakiwa kuwa na vigezo vifuatavyo wakizingatia vigezo vikuu kumi vilivyotajwa hapa chini;
- Umri usiopungua miaka 25 na usiozidi miaka 45
- Elimu ya kidato cha nne na kuendelea
- Cheti cha ujuzi wa udereva wa magari makubwa kutoka NIT/VETA
- Cheti kinachomruhusu dereva kubeba mizigo na bidhaa mbalimbali kwa malori
- Barua ya uhakiki alama za vidole kutoka polisi
- Afya inayostahimili safari za nje na ndani ya nchi
- Nyaraka za kusafiria (Passport Kubwa)
- Uwezo wa kusoma na kuandika kwa ufasaha
- Uzoefu wa kuendesha magari makubwa usiopunuga miaka mitano
- Leseni ya udereva yenye sifa ya kuendesha magari makubwa
Maombi yote yaletwe ofisini kwetu kuanzia tarehe 26-08-2021 kwa njia ya mkono na kukabidhiwa kwa walinzi wetu, na kujaza kwenye fomu maalumu. Ofisi zetu zipo Shimo la Udongo, kiwanja namba 2084, Mandela Road Kurasini, Mkabala na maegesho ya magari shimo la udongo. Maombi yote yaelekezwe kwa
Meneja Rasilimali Watu
GALCO LIMITED
S.L.P 6244, DAR ES SALAAM
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 23-09-2021
Zingatia – Muhimu
- Watakaochaguliwa watapigiwa simu na Ofisi kwa mchakato Zaidi
- Epuka kutapeliwa fedha au kitu chochote cha thamani kwa ahadi ya kupata upendeleo wa ajira ndani ya GALCO LIMITED.