Mhasibu BET - SACCOS LTD Dar es Salaam
Full-Time
30th June 2018
2105

BET SACCOS Ltd ni Chama cha Ushirika cha akiba na mikopo kilichoanzishwa chini ya sheria ya Vyama vya ushirika Na. 6 ya mwaka 2013. Madhumuni ya chama hiki ni kutoa huduma bora za kifedha ikiwemo kuweka akiba, amana na huduma za mikopo kwa masharti nafuu kwa wanachama wake. BET SACCOS inatanganza nafasi ya kazi ya mhasibu

 

Ataripoti Kwa: Bodi ya BET -  SACCOS LTD

Eneo: Uwanja wa Maonyesho wa Mwl. J.K Nyerere

Mshahara: Kulingana na Scheme ya BET SACCOS LTD

Mkataba wa ajira: Mwaka Mmoja

Ofisi ilipo: Dar es Salaam

Umri: usiyozidi miaka 35

 

Majukumu

  • Kuandaa bajeti za miradi na chama
  • Kusimamia maswala yote ya uendeshaji wa miradi
  • Kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi ya miradi na chama
  • Kusimamia mali za miradi kulingana na miongozo iliyopo
  • Kusimamia uhakiki wa vitabu vya kihasibu, nyaraka mbalimbali za manunuzi ya bidhaa za miradi na kuwasilisha kwa wakati
  • Kuwajibika kujibu hoja za wakaguzi
  • Kushauri na kuanzisha mfumo wa kihasibu wa vyama vya ushirika na kuingiza taarifa na nyaraka kwenye mfumo
  • Kusimamia na kutekeleza maamuzi yote ya kamati ya mradi
  • Kushiriki vikao vya kamati ya miradi na vile vitakavyoamuliwa
  • Kuandaa taarifa za utendaji siku, wiki, mwezi, robo mwaka na chama na mradi
  • Kuandaa malipo ya wafanyakazi wa mradi na makato ya kila mwezi
  • Kutekeleza kazi nyingine atakazopangiwa na viongozi wake

Sifa za Mwombaji

Mwombaji anatakiwa awe na shahada ya uhasibu, biashara au uchumi

 

Uzoefu/Masharti ya Ajira

  • Awe amefanya kazi katika vyama vya ushirika zaidi ya miaka miwili
  • Awe na ujuzi wa kutumia mifumo ya uhasibu
  • Awe na uwezo wa kutekeleza kazi bila kusimamiwa
  • Awe na uwezo kutekeleza maswala mbalimbali yanayohusu vyama vya ushirika
  • Awe mwadilifu na mwenye juhudi ya kazi na kujituma kwa bidii na kuhamasisha wenzake kazini
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi hata muda wa ziada
  • Awe mwadilifu na mwenye nidhamu ya kazi
  • Awe na uwezo wa kusimamia miradi
  • Awe na uwezo wa kubuni na kung’amua matokeo chanya kwa chama pamoja na kufanya uchambuzi wa gharama na faida(cost benefit analysis)

Maombi ya tumwe kabla ya tarehe 30 juni, 2018, Saa 10:00 Jioni kwa;

Mwenyekiti,

BET - SACCOS LTD,

Uwanja wa Maonyesho wa Mwl. J.K Nyerere

S.L.P 5402, DAR ES SALAAM

Application

Sorry, this job no longer accepts new applications.