Mhasibu Msaidizi
Lulu Saccos Ltd
Mbeya
Full-Time
18th July 2018
Bodi ya chama cha ushirika wa akiba na mikopo Lulu(Lulu Saccos Ltd) MBR.737 kilichopo Jiji la Mbeaya maeneo ya Soweto kata ya Ruanda kinatoa tangazo la kazi kwa nafasi zifuatazo:-
Mhasibu Msaidizi - Nafasi 1
Sifa
- Awe na umri kuanzia 23 hadi 40
- Awe na elimu ya sekondari
- Awe na stashahada ya uhasibu na ushirika
- Awe ni mtanzania anayeishi katika Jiji la Mbeya
- Awe hajawahi kufukuwa kazi mahala popote kwa kosa la jinai
- Awe mtu wa kujituma
- Awe anajua kutumia kompyuta
- Awe mtu anayejisimamia mwenyewe
- Awe ni mzaliwa/mwenyeji wa mkoa wa Mbeya
Kazi
- Kusimamia na kuratibu shuguli zote za makarani wa fedha
- Kuandika na kutunza vitabu na kumbukumbu nyingine za fedha
- Kupokea malinganisho ya hesabu ya benki ya kila siku
- Kuandaa taarifa ya fedha ya kila mwezi
- Kufunga vitabu vya hesabu za chama na kuziwasilisha kwa mhasibu wa chama
- Atawajibika kwa mhasibu wa chama
- Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na mwajiri wake
- Kazi hii ni ya mkataba wa miaka miwili
Utaratibu wa kuomba
- Mwombaji anatakiwa kuambatanisha picha mbili passport size
- Mwombaji atatakiwa kuambatanisha vivuli vya vyeti vya kuzaliwa na vya masomo
- Mwombaji aambatanishe CV yake wakati wa kuomba kazi
- Mwombaji aonyeshe mawasiliano yake bayana
- Mwombaji atakayefaulu kwa awamu ya kwanza ataitwa kwenye usaili
- Mwombaji atakeyeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili
- Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usaili
- Maombi yatumwe kwa:-
MWENYEKITI WA BODI
CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO LULU
S.L.P 3467
MBEYA