Mhudumu wa Ofisi
GoodNeighbors International
Mbozi, Songwe, Tanzania
Full-Time
14th August 2021
Shirika la Good Neighbors Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali linatoa huduma na misaada kwa jamii kupitia sekta za elimu, afya, utetezi wa haki za Watoto, elimu ya usafi na maji na kukuza kipato miongoni mwa wanajamii ili kufanikisha maendeleo ya jamii husika
Good Neighbors Tanzania, inakaribish maombi kwa watanzania wenhe sifa na uwezo wa kujana nafasi moja ya mhudumu wa ofisi ya Nambinzo iliyopo Kijiji cha Isenzanya wilayani Mbozi, Mkoa wa Songwe
Majukumu ya Kazi
- Kufanua usafi wa Ofisi kwa ujumla (nje na ndani) pamoja na kuzingaia matumizi mazuri ya vifaa vya usafi
- Kuweka kumbukumbu ya vifaa vyote vya usafi
- Kupanda na kumwagilia maua kuzunguka Ofisi
- Kupanga mafile na vifaa vya Ofisi kwa muonekano mzuri na wa kuvutia
- Kutoa taarifa za awali ikiwa kuna uhitaji wa kununua vifaa vya usafi
- Kupokea na kukaribisha wageni
- Kupokean nyaraka za Ofisi na kuhakikisha unaifikisha kwa mhusika kwa ajili ya ufuatiliaji
Masharti ya Jumla
- Muombaji awe raia wa Tanzania na wenye umri usiopungua miaka 18
- Muombaji lazima awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea
- Muombaji awasilishe barua ya maombi ya kazi kwa nafasi tajwa yenye maelezo binafsi yanayojitosheleza, anwani, namba za simu za kuaminika Pamoja na majina ya wadhamini watatau wa kuaminika
- Barua ya maombi iandikwa kwenda kwa Mkurugenzi mkaazi, shirika la Good Neighbors Tanzania, S.L.P 292, Mbozi
- Muombaji aambatanishe pia nakala ya cheti cha kuhitimu (leaving certificate) ya kidato cha nne
- Maombi yaandikwe kwa lugha ya kiswahili na yawasilishwe, katika Ofisi ya Good Neighbors iliyopo Kijiji cha Isenzanya
- Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 14 Agasti 2021 saa Kumi Kamili (10:00) jioni
Muda wa kufanya kazi ni Jumatatu mpaka Ijumaa, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi [12:00] mpaka saa saba kamili [7:00] mchana.