Mpishi Maternity Africa Arusha, Tanzania
Full-Time
6th February 2022

MA/HR/KSS/01/22 

Maternity Africa ni taasisi isiyo ya kiserikali inayohusika na afya ya uzazi kwa kina mama yenye malengo ya kutoa huduma za matibabu kwa wanawake wenye hali duni kiuchumi wakati wa kujifungua, kutoa elimu na huduma ya uzazi wa mpango na kutibu matatizo yanayotokana na uzazi ikiwemo Fistula

Tunatazamia kuajiri Mpishi mwenye uzoefu wa kazi, ueledi, maadili ya kazi, na atakayeweza kuendana na sera na maadili ya taasisi yetu

Majukumu ya kazi

  • Ujuzi na uwezo wa kupika na kuaandaa chakula cha watu wengi
  • Uwezo wa kupika vyakula vya asili ya Kitanzania
  • Kuweka rekodi ya stoku ya vyakula vinavyoingia na kutoka jikoni
  • Kutunza mazingira ya jikoni na kuzingatia usafi katika maandalizi ya vyakula
  • Kufanya makadirio ya chakula kitakachotosha/hitajika kulingana na idadi ya watu
  • Kuosha vyombo na vifaa vyote vitakavyotumika wakati wa kupika na baada ya watu kutumia
  • Kuhakikisha mazingira ya usalama katika maeneo ya kazi
  • Kufanya kazi ingine yeyote utakayoagiziwa na msimazi wako

Vigezo 

Cheti cha Sekondari (O-level) Cheti cha kuhitimu mafunzo ya juu katika taaluma ya Upishi au hotel Management. Uzoefu wa Miaka Mitatu (3) ya kazi ya upishi katika taasisi inayopika chakula cha watu zaidi ya 150. Uwezo wa kufanya kazi kwa shifti ya mchana na usiku

Jinsi ya kutuma maombi ya Kazi 

Tuma maombi yako kupitia barua pepe recruitment@maternityafrica.org. Tarehe ya mwisho kupokea barua za maombi ya kazi ni tarehe 06/02/2022. Usipopigiwa simu baada ya wiki Moja tangu tangazo hili kufungwa, tafadhali tambua kua hujafanikia kuchaguliwa katika orodha ya watahiniwa.

Application

Sorry, this job no longer accepts new applications.