Mwanasheria Chama cha Walimu Tanzania(CWT) Tanzania
Full-Time
21st December 2018

Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ni Chama cha Wafanyakazi kutoka kada ya Walimu ambacho shughuli zake zipo Tanzania Bara tu. Chama kimesajiliwa kwa Namba 004 chini ya Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini Namba 6 ya mwaka 2004 na kinaajiri Wafanyakazi kwa ajira ya kudumu ambao wapo katika kila Mikoa, Wilaya na Makao Makuu. Ili kuboresha huduma kwa Wanachama, CWT kinatoa nafasi ya ajira kwa Mtanzanla mwenye sifa ya Elimu ya Sheria katika ofisi za Chama Makao Makuu yaliyopo Jijini Dodoma.

MWANASHERIA -NAFASI 1

Sifa za mwombaji

  • Awe na Shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali na awe ameapishwa kuwa Wakili
  • Awe na uwezo wa kuongea kwa ufasaha na kuandika lugha ya Kiswahili na Kiingereza
  • Awe na uwezo wa kutumia kompyuta
  • Awe raia wa Tanzania 

Majukumu ya kazi

  • Kutoa ushauri wa kisheria kwa Walimu na Chama
  • Kutatua migogoro ya kikazi wanayokabiliana nayo Walimu
  • Kufuatilia suluhu ya maatizo mbalimbali ya Walimu katika ofisi mbalimbali za Serikali na Waajiri
  • Kuandaa taarifa ya kazi za Idara za robo mwaka, nusu mwaka na Mwaka mzima Kuandaa bajeti ya Idara
  • Kuhakikisha Idara Inapata makala mbalimbali za kisheria
  • Kufuatilia na kupata mabadiliko mbalimbali ya Sheria (Amendments) pamoja na Gazeti la Serikali (Government Gazette)
  • Kufuatilia upatikanaji wa hukumu za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa (Authorities)
  • Kutunza Maktaba ya mambo ya Sheria Kufanya kazi nyingine atakazotumwa na Katibu

 

MASHARTI YA JUMLA

  1. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
  2. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa
  3. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed CV) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika
  4. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea
  5. Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI
  6. Vyeti vya kitaaluma
  7. Picha moja 'passport size'ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma
  8. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA)
  9. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi
  10. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria
  11. Maombi yanaweza kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza
  12. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 21 Desemba, 2018 saa 10.00 Jioni kupitia anuani ifuatayo:

Katibu Mkuu,

Chama cha Walimu Tanzania,

S.L.P. 3077,

DODOMA.

Barua pepe: Info@ttu.or.tz

Imetolewa na:

Mwl. Deus G. Self KATIBU MKUU - CWT



Application

Sorry, this job no longer accepts new applications.